-
-
by
Victor Abuso
Kumekuwa na hisia mseto nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya TP Mazembe kufungwa katika hatua ya robo fainali kuwania ubingwa wa kombe la dunia baina ya vlabu.
Baadhi ya mashabiki wanahisi kuwa maanadalizi ya TP Mazembe hayakuwa mazuri kuelekea michuano hiyo huku wengine wakidokeza kuwa ilikuwa ni tu bahati mbaya kwa timu yao kufungwa.
Mchambuzi wa soka na mwandishi wa Habari wa AFP Lucien Kahozi Koshia ameiambia soka25east.com akiwa mjini Osaka kuwa, wachezaji wa Mazembe walilemewa na kasi ya Sanfrecce Hiroshima.
Mazembe walionesha mchezo mzuri katika mechi zilizopita lakini pia katika mchuano wa robo fainali na licha ya kupata kona saba walishindwa kutumia nafasi hizo kupata ushindi.
“Wachezaji wa Mazembe wanaotoka nchi nane barani Afrika hawakuwa na mazoezi ya pamoja, hali ya hewa ilikuwa nzuri hapa Japan lakini Mazembe walilemewa,” alisema Kahozi.
Aidha, kwa mujibu wa Kahozi kutokuwepo kwa kipa wa siku nyingi na mwenye uzoefu mkubwa Robert Kidiaba, huenda kulichangia Mazembe kufungwa.
“Naamini kama Kidiaba angekuwa langoni, mambo yangekuwa tofauti.Kidiaba hapa Japan walikuwa wanamwongopa sana na hata nilishuhudia jezi yake ikiteketezwa moto,” aliongeza Kahozi.
TP Mazembe sasa itachuana na Cub America ya Mexico siku ya Jumatano kutafuta mshindi wa nafasi ya tano katika mashindano hayo.
Mapema siku ya Jumapili, Club America ilipoteza katika hatua ya robo fainali baada ya kufungwa na Guangzhou Evergrande ya China kwa mabao 2 kwa 1.
Michuano ya nusu fainali ni siku ya Alhamisi, Barcelona watachuana na Guangzhou Evergrande ya China huku Sanfrecce Hiroshima ya Japan ikichuana River Plate kutoka Argetina.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...