Connect with us

Uchambuzi: Wakenya washindwa kutamba katika ligi ya Tanzania bara

Uchambuzi: Wakenya washindwa kutamba katika ligi ya Tanzania bara

Na Victor Abuso

Klabu ya Yanga FC inayoshiriki katika ligi kuu ya Tanzania bara, imeonesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Gor Mahia ya Kenya Michael Olunga.

Wapambe wa klabu ya Yanga wamekuwa wakimchungulia Olunga kwa umakini mkubwa kutokana na ushupavu wake katika michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya kuonekana kuisaidia klabu yake kupata ushindi.

Mbali na Olunga, mchezaji mwingine wa Kenya ambaye hakuwepo katika michuano hii lakini amesajiliwa na klabu nyingine ya Tanzania Azam FC ni Allan Wanga, mchezaji wa zamani wa klabu ya Al-Merreikh ya Sudan.

Hata hivyo katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na wasiwasi kuhusu kiwango cha wachezaji kutoka nchini Kenya pindi wanapojiunga na vlabu vya Tanzania bara kinyume na ilivyokuwa hapo awali.

Wachezaji kutoka nchini Kenya wanaokumbukwa sana na mashabiki wa soka nchini Tanzania waliofanya vizuri ni pamoja na Boniface Ambani ambaye wakati akiichezea klabu ya Yanga aliifungia mabao 18 wakati wa msimu wa mwaka 2009 na kuwa mfungaji bora.

Wakenya wengine wanaokumbukwa kufanya vizuri katika soka la Tanzania ni pamoja na Maurice Sunguti, Bernard Mwalala, John Baraza, Mike Barasa, Edwin Mkenya, Pascal Ochieng na Joseph Shikokoti katika nyakati tofauti.

Mashabiki wa klabu ya Simba, hawajawahi kuwasahau Mark Sirengo aliyeichezea klabu hiyo ya wekundu wa Msimbazi katika msimu wa mwaka wa 2002/2003, pamoja na Hillary Echesa aliyeicheza msimu wa mwaka 2010.

Mafanikio ya wachezaji kutoka Kenya katika siku za hivi karibuni yamepungua kwa kiasi kikubwa sana huku wachezaji kama Paul Kiongera, Humphrey Mieno, Joakins Atudo, Osborne Monday wakishindwa kufanya vizuri katika ligi ya Tanzania bara.

Kiongera ambaye alionekana kuwa shupavu wakati akiichezea Gor Mahia na KCB nchini Kenya, alipata jeraha baya wakati klabu yake ya Simba FC mwaka 2014 ilipokuwa inamenyana na Coastal Union jeraha ambalo lilimweka nje ya uwanja muda mrefu.

Atudo na Mieno ambao walikuwa wanaichezea Azam FC waliondoka katika mazingira ya kutatanisha baada ya msimu mmoja katika klabu hiyo.

Mganda Danny Serenkumma aliyekuwa mfungaji bora katika klabu ya Gor Mahia mwaka 2014, alipokuja Simba alijikuta mambo yanakuwa magumu na kuamua kuondoka sawa na mchezaji wa sasa wa Gor Mahia George “Blackberry” Odhiambo.

Rama Salim naye anayeichezea Coastal Union hawajawa na msimu wa kuridhisha katika klabu yake ikilinganishwa wakati akiwa Gor Mahia na Bandari.

Imekuwa ni vigumu kubaini ni kwanini wachezaji kutoka Kenya hawafanyi vizuri kama ilivyokuwa hapo awali licha ya kulipwa vizuri na vlabu vya Tanzania.

Je, ikiwa Olunga atajiunga na Yanga hali itakuwaje ? Allan Wanga naye Azam FC atafanikiwa na kuwa kama Boniface Ambani ?

Ex- CAF Media Expert. An expert on African football with over 15 years experience ,always with an ear to the ground with indepth knowledge of the game. I have worked for top publications including 7 years at www.supersport.com until i founded www.soka25east.com to quench the thirst of football lovers across the continent. I have trained young upcoming journalists who are now a voice in African football.I have covered World Cup,AFCON,CHAN,Champions League,Confederations Cup,Cecafa,Cosafa,Wafu and many other football tournaments across the World. Founder Football Africa Arena(FAA),Founder www.afrisportdigital.com

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in