Timu ya taifa ya soka ya Uganda, inaanza mazoezi hivi leo katika uwanja wa Kabira, kuelekea mechi muhimu kufuzu kucheza fainali ya bara Afrika dhidi ya Lesotho siku ya Jumapili.
Tayari kocha Sebastien Desabre amekitaja kikosi cha wachezaji 24 kuanza maandalizi ya mchuano huo muhimu.
Kabla ya mechi dhidi ya Lesotho, Uganda Cranes itakuwa na mechi za kirafiki dhidi ya timu za taifa chini ya umri wa miaka 17, 20 na 23. Mechi hizo zitachezwa katika uwanja wa Lugogo jijini Kampala.
Uganda ilianza vema kampeni hii kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cape Verde, na kutoka sare ya kutofungana na Tanzania katika kundi L .
Wachezaji walioitwa ni pamoja na:-
Denis Onyango, Jamal Salim, Charles Lukwago, Murushid Juuko, Isaac Isinde, Timothy Awanyi, Denis Iguma, Nicholas Wadada, Godfrey Walusimbi, Isaac Muleme, Joseph Ochaya.
Wengine ni pamoja na Hassan Wasswa, Ibrahim Sadaam, Taddeo Lwanga, Moses Waisswa, Khalid Aucho, Allan Kateregga, Faruku Miya, Emma Okwi, Edris Lubega, Derrick Nsibambi, Milton Karisa, Allan Kyambadde na Patrick Kaddu.