Na Victor Abuso,
Timu ya taifa ya soka ya Uganda imeanza mazoezi katika uwanja wa Kimataifa wa Namboole jijini Kampala tayari kwa michuno ya kufuzu katika fainali za mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2017 nchini Gabon.
Kocha Milutin ‘Micho’ Sredojevic ameanza mazoezi hayo na wachezaji 14 kwa maandalizi ya mchuano wa kwanza dhidi ya Bostwana mwishoni mwa juma hili jijini Kampala.
Uganda imepangwa pia katika kundi moja na Burkina Faso na Comoros.

Pamoja na maandalizi hayo, Uganda Cranes pia inajiandaa katika michuano ya kufuzu ya Afrika baina ya wachezaji wa ndani CHAN itakayofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.
Vijana hao wa Micho wamepangiwa kwa mara nyingine kupambana na Tanzania nyumbani na ugenini tarehe 21 mwezi huu kabla ya kurudiana tena mwezi Julai.
Kikosi kinachojiandaa kwa michuano ya CHAN:-
Brian Bwete, Mathias Kigonya, Alex Kitata, Kiyemba Ibrahim, Eturude Abel,Ntambi Julius,Katongole Henry, Okello Sylvester, Bukenya Deus, Farouk Musisi, Fahad Muhammed Toko, Mutyaba Muzamil, Paul Mbowa na Frank Kalanda.
Mbali na Uganda mataifa mengine ya Afrika Mashariki na Kati yanayojiandaa kufuzu michuano hiyo ya CHAN ni pamoja na Djibouti itakayomenyana na Burundi na Ethiopia na Kenya.
Washindi katika hatua hii watafuzu katika mzunguko wa kwanza kujiunga na Sudan ambayo imekwishafuzu.
Rwanda wamefuzu kwa sababu ni wenyeji wa michuano hii.amoja na maandalizi hayo, Uganda Cranes pia inajiandaa katika michuano ya kufuzu ya Afrika baina ya wachezaji wa ndani CHAN itakayofanyika jijini Kigali nchini Rwanda.
Vijana hao wa Micho wamepangiwa kwa mara nyingine kupambana na Tanzania nyumbani na ugenini tarehe 21 mwezi huu kabla ya kurudiana tena mwezi julai