Na Victor Abuso, Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wasiozidi miaka 23 imefuzu katika mzunguko wa tatu kuwania tiketi ya kufuzu katika michuano ya Afrika itakayopigwa nchini Senegal kati ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 12 Desemba mwaka huu. Uganda ndio timu pekee inayowakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika michuano hiyo ya vijana na ilifuzu baada ya kuishinda Rwanda kwa jumla ya mabao 4 kwa 1. Vijana hao wanaofahamika kwa jina maarufu Uganda Kobs, walipata ushindi nyumbani na ugenini na mwishoni mwa juma lililopita, wakiwa katika uwanja wa nyumbani wa Nakivubo jijiji Kampala ilipata ushindi wa mabao 2 kwa 0. Mabao ya Uganda yalitiwa kimyani na nahodha John Ssemazi na Faruku Miya kipindi cha pili cha mchuano huo. Uganda sasa itamenyana na Misri nyumbani na ugenini mwezi katikati na mwisho mwa mwezi ujao.
Vikosi vya timu:
Uganda :
Salim Magoola (G.K), Dues Bukenya, Brian Ochwo, Shafik Bakaki, Richard Kasagga, Derrick Tekkwo, Kizito Kezironi,Faruku Miya, Fahad Muhammed Tokko, John Ssemazi
Wachezaji wa akiba : 54’ Yunus Sentamu In, Hassan Muhammed Fahad Out, 58’ Muzamiru Mutyaba In, Kezironi Kizito Out, 69’ Martin Kizza In, John Ssemazi
James Alitho (G.K), Tom Matisko, Abel Eturide and Ibrahim Kiyemba
Rwanda :
Marcel Nzarora (G.K), Michel Rusheshangoga, Celestin Ndayishimye, Faustin Usengimana, Emery Bayisenge, Yannick Mukunzi, Bonfils Kabanda, Andrew Buteera, Djihad Bizimana, Xavio Nshuti, Isaie Songa
Wachezaji wa akiba: 26’ Michel Rusheshangoga Out, Fitina Ombarenga In, 65’ Andrew Butera Out, Kevin Muhiire Gahungu Habarurema (G.K), Bienvenue Mugenzi, Antoine Ndayishimiye , Abdoul Rwatubyaye, Robert Ndatimana
Mataifa mengine ya Afrika Mashariki yaliyoondolewa katika michuano hii mbali na Rwanda ni Kenya na Somalia.
Mataifa manane yatashiriki katika michuano ya Afrika na yatakayomaliza katika nafasi tatu bora yatafuzu katika michuano ya Olimpiki mwaka ujao.