Misri imerejea kileleni mwa kundi E katika michuano ya soka kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.
Hatua hii ilikuja baada ya Misri kuifunga Uganda bao 1-0 katika mchuano muhimu uliochezwa katika uwanja wa Borg El-Arab mjini Alexandria Jumanne usiku.
Bao la mshambuliaji Mohamed Salah katika dakika ya saba ya mchuano huo kipindi cha kwanza, ilitosha kuisaidia Misri kumaliza mechi hiyo kwa ushindi huo mwembamba lakini muhimu.
Kuelekea katika mchuano huo, Uganda waliishinda Misri mabao 2-1 wiki iliyopita jijini Kampala.
Ushindi huo umewapa furaha kubwa mashabiki wa Misri ambao mara ya mwisho kufuzu katika fainali ya kombe la dunia ni mwaka 1990.
Baada ya mechi nne, Misri inaongoza kundi hili kwa alama 9, Uganda ni ya pili kwa alama 7, Ghana ya tatu kwa alama 5 huku Congo Brazaville ikiwa ya mwisho kwa alama 1.
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishindwa kuongoza kundi A baada ya kukubali sare ya mabao 2-2 dhidi ya Tunisia jijini Kinshasa.
Leopard ilianza vema sana baada ya kupata bao la mapema katika dakika ya tisa kipindi cha kwanza kupitia mchezaji wake Chancel Mbemba huku Paul-Jose M’poku akifunga bao la pili katika dakika ya 48.
Hata hivyo, kipindi cha pili mambo yalibadilika baada ya Mohamed Amine Ben Amor kufunga bao katika dakika ya 78 huku Anice Badri akisawazisha katika dakika ya 79.
Matokeo kamili:-
Algeria 0-1 Zambia
Mali 0-0 Morocco
Misri 1-0 Uganda
DR Congo 2-2 Tunisia
Burkina Faso 2-2 Senegal
Cote d’Ivire 1-2 Gabon
Afrika Kusini 1-2 Cape Verde
Congo 1-5 Ghana
Ratiba Oktoba 7 2017
Kundi A
Guinea vs Tunisia
Libya vs DR Congo
Kundi B
Nigeria vs Zambia
Cameroon vs Algeria
Kundi C
Mali vs Ivory Coast-Oktoba 6 2017
Morocco vs Gabon
Kundi D
Afrika Kusini vs Burkina Faso
Caper Verde vs Senegal
Kundi E
Uganda vs Ghana
Misri vs Congo-Oktoba tarehe 8 2017
Michuano yote ya makundi itamalizika tarehe 6 mwezi Novemba.