Connect with us

Nchi ya Uhispania inaomba ushirikiano na Ureno ili kwa pamoja kuwa wenyeji wa kombe la dunia mwaka 2030.

Ombi hili, limetolewa na Waziri Mkuu wa Uhispania Pedro Sanchez wakati akiwa ziarani nchini Morocco siku ya Jumatatu.

Magazeti nchini Uhispania yanaripoti kuwa Morocco imekubali ombi hilo.

Uhispania imewahi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia mara moja, mwaka 1982.

Morocco imejaribu kuomba kuwa mwenyeji wa kombe la dunia ya mwaka 1994, 1998, 2006, 2010 na 2026 bila mafanikio.

 

More in