Uingereza imekuwa nchi ya mwisho kuwa miongoni mwa mataifa nane, yatakayocheza katika hatua ya robo fainali, kuwania fainali ya kombe la dunia inayoendelea nchini Urusi.
Hatua hii ilikuja baada ya kushinda kwa mikwaju ya penalti 3-4 dhidi ya Colombia katika mchuano wenye ushindani mkali Jumatano usiku.
Kuelekea mwisho wa mchuano huo, bao la nahodha Harry Kane, lilionekana kuipa ushindi Uingereza lakini mambo yalibadilika wakati wa muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za kawaida wakati Yerri Mina ilipoisawazia Colombia.
Matokeo hayo, yaliyalazimisha mataifa hayo kwenda katika muda wa ziada wa dakika 30 na baadaye mikwaju ya penalti baada ya muda kumalizika kwa mchuano huo kusalia kwa sare ya bao 1-1.
Andres Uribe na Carlos Bacca, walishindwa kufunga mikwaju sawa na Jordan Henerson wa Uingereza, lakini wachezaji wanne waliosalia walihakikisha kuwa wanatikisa nyavu ya Colombia.
Penalti za Uingereza zilifunwga na nahodha Harry Kane, Marcus Rashford,Kieran Trippier na Eric Dier.
Mchuano mwingine wa mwondoano siku ya Jumanne, bao pekee la Emil Forsberg liliiwezesha Sweden kufuzu katika hatua ya robo fainali dhidi ya Uswisi katika uwanja wa Krestovsky mjini Saint Petersburg.
Ratiba kamili ya michuano ya robo fainali:-
Ijumaa, Julai 6 2018
Uruguay vs Ufaransa
Brazil vs Ubelgiji
Jumamosi, Julai 7 2018
Sweden vs Uingereza
Urusi vs Croatia