Connect with us

Urusi 2018: Burundi yafuzu mzunguko wa pili

Urusi 2018: Burundi yafuzu mzunguko wa pili

Timu ya taifa ya soka ya Burundi, Intamba Murugamba imeungana na Kenya, Tanzania na Ethiopia kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati kufuzu katika hatua ya pili ya kufuzu katika fainali ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Burundi ilijihakikishia nafasi hiyo siku ya Jumanne, baada ya kuifunga Ushelisheli mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa marudiano uliochezwa jana jijini Bujumbura.

Mchuano huo ulisimamishwa kwa muda kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jijini Bujumbura na viunga vyake lakini ukarejelewa tena baada mvua kumalizika na kufuzu kwa jumla ya mabao 3 kwa 0.

Burundi sasa inajiandaa kumenyana na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchuano wa mzunguko wa pili nyumbani na ugenini katikati ya mwezi wa Novemba.

Wawakilishi wengine wa eneo la Afrika Mashariki Sudan Kusini, ambao waliweka historia kwa kushiriki kwa mara ya kwanza katika michuano hii ya kufuzu, waliondolewa na Mauritania baada ya kufungwa kwa jumla ya mabao 5 kwa 1 licha ya kutoka sare ya moja kwa moja jijini Juba.

Somalia pia iliondolewa na Niger kwa kufungwa jumla ya mabao 6 kwa 0 nyumbani na ugenini.

Kenya itacheza na Cape Verde, huku Tanzania ikimenyana na Algeria katika mzunguko huo wa pili.

Uganda na Rwanda tayari zilikuwa zimefuzu katika hatua hii ya pili.

Mshindi wa mzunguko wa pili atafuzu katika hatua ya makundi.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in