Kocha wa TP Mazembe Pamhile Mihayo ameanza vyema harakati za kuwania ubingwa wa Afrika kwa ngazi ya klabu baada ya kikosi chake hapo jana kuishindilia ES Setif ya Algeria kwa mabao 4-1.
Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Frederick Kibassa Mjini Lubumbashi na unakuwa mwanzo mwema kwa klabu hiyo hiyo ambao ilikosekana katika hatua ya makundi kwa misimu miwili.
Mzembe pia itachuana na timu za Difaa Al Jadida na MC Alger katika kundi B ikiwania kufuzu hatua ya robo fainali tangu ilipofanya hivyo mwaka 2015, ambapo moja kwa moja ilikwenda kuchukua ubingwa.
Uzoefu wa nathan Sinkala
Sinkala ni mchezaji kutoka Zambia ambaye amekuwa na msaada mkubwa kwa Mazembe katika zaidi ya misimu sita aliyocheza klabu hapo.Uzoefu wake katika michuano hii akisaidiana na akina Rainford Kalaba utakuwa na manufaa makubwa kwa Mazembe katika michezo ya kundi B.
Wapinzani wao
Wapinzani wa Mazembe katika kundi hili ni wapinzani wa kweli, ni lazima ishinde mechi zote za nyumbani. Difaa ni klabu nzuri na imeonyesha hivyo katika mchezo wa kwanza ilipotoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na MC Alger.
Nafasi kwa Mazembe
Kama wataendelea na kasi hii katika mechi za nyumbani nina imani TP Mazembe itamaliza katika nafasi mbili za juu katika kundi B na hivyo kutinga hatua ya robo fainali