Maafisa wakuu wa Shirikisho la soka barani Afrika CAF wako ziarani nchini Kenya kuthathmini maandalizi ya nchi hiyo kuandaa michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza katika ligi za nyumbani CHAN mwaka 2018.
Uongozi wa soka nchini Kenya umethibitisha uwepo wa Makamu wa kwanza wa rais wa CAF Suketu Patel na Katibu Mkuu Hicham El Amrani.
Wawili hao wanatembelea viwanja vitakavyotumiwa kuandaa michuano hiyo lakini pia hoteli zitakazotumiwa na wachezaji pamoja na wageni wengine mashuhuri.
Viwanja vinavyotarajiwa kuandaa michuano hiyo ni pamoja na ule wa Kimataifa wa Moi Kasarani na Nyayo jijini Nairobi, Uwanja wa Moi mjini Kisumu, Mbaraki mjini Mombasa na Kinoru mjini Meru.
Rais wa FKF Nick Mwendwa, na naibu wake Doris Petra, wanaandama na ujumbe huo wa CAF.