Al-Merrikh ya Sudan, KCCA ya Uganda, AS Vita Club ya DRC na Yanga ya Tanzania zimefuzu katika mzunguko wa kwanza kuwania taji la klabu bingwa barani Afrika mwaka 2017.
Vlabu hivi vilifuzu baada ya kumalizika kwa michuano ya marudiano hatua ya wali mwishoni mwa wiki iliyopita, zilizopigwa katika viwanja mbalimbali barani Afrika.
Michuano ya mzunguko wa kwanza, itachezwa mwezi Machi nyumbani na ugenini na mshindi atafuzu katika hatua ya makundi.
KCCA itamenyana na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ambao ndio mabingwa watetezi wa taji hili, huku Rivers United ya Nigeria ikimenyana na Al-Merrikh ya Sudan.
Yanga ya Tanzania itamenyana na Zanaco ya Zambia. Zanaco ilifuzu baada ya kuishinda APR ya Rwanda katika hatua ya awali.
AS Vita Club nayo itatafuta nafasi ya kufuzu na itamenyana na Gambia Ports Authority huku TP Mazembe ya DRC ikimenyana na CAPS United ya Zimbabwe.
Ratiba nyingine ya michuano ya klabu bingwa:-
Al-Hilal vs AS Port-Louis 2000
AC Leopards vs Saint George
Al-Ahly vs Bidvest Wits
Coton Sport vs CnaPS Sport
Zamalek vs Enugu Rangers
Ferroviario Beira vs Stade Malien
Wydad Casablanca vs CF Mounana
Al-Ahli Tripoli vs FUS Rabat
Esperance de Tunis vs Horoya
Etoile du Sahel vs AS Tanda
USM Alger vs Rail Club du Kadiogo
Vlabu 16 vitafuzu katika hatua ya makundi na kugawanywa katika makundi manne, kila kundi na vlabu vinne.