Connect with us

Wachezaji wa Eritrea Cecafa U-20 wazamia Jinja Uganda

Wachezaji wa Eritrea Cecafa U-20 wazamia Jinja Uganda

Na Mwandishi Wetu akiwa Uganda,

Jumamosi ya Oktoba 5 2019 ilikuwa siku ya kumalizika kwa michuano ya CECAFA U-20, mashindano hayo yaliitimishwa kwa michezo miwili.

Mchezo wa kwanza ulikuwa wa Eritrea walioshinda 1-0 dhidi ya Sudan na kuibuka washindi wa tatu wa mashindano na mchezo wa pili ni Tanzania dhidi ya Kenya, Tanzania ikishinda 1-0 na kuwa Mabingwa.

Habari kubwa na kushitua ilikuwa ni kutoka katika timu ya Eritrea ambapo timu yao baada ya kupoteza nusu fainali wachezaji wao wanaotajwa kufikia watano walitoroka kambini tukio ambalo linadaiwa ni kuzamia kutokana  na hulka ya wachezaji hao.

Kitu ambacho kilipelekea wachezaji wa Eritrea kuwekewa ulinzi mkali baada ya kuisha mchezo ili kudhibiti wachezaji 15 waliosalia kati ya 20 wasitorokea, inadaiwa kuwa hii sio mara ya kwanza kwa wachezaji wa Eritra kutoroka baada ya mashindano kwa sababu ya ugumu wa maisha katika taifa lao wakiamini njia sahihi ya wao kupata mafanikio ya kimaisha ni kuzamia katika baadhi ya nchi baada ya mashindano ya CECAFA kumalizika.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in