Connect with us

Wachezaji wa kigeni watia fora ligi ya Tanzania bara

Wachezaji wa kigeni watia fora ligi ya Tanzania bara

Ligi kuu nchini Tanzania ikielekea kufika mwisho, vlabu vitatu vya Yanga FC, Azam FC na Simba FC viliwasajili idadi kubwa ya wachezaji wa kigeni kuwasaidia kufanya vizuri msimu huu.

Hii imedhirika baada ya Amis Tambwe kutoka Burundi kuongoza katika safu ya ufungaji wa mabao, na kuelekea mchuano wa mwisho msimu huu, ameifungia timu yake ya Yanga mabao 21.

Hamis Kizza anayechezea Simba SC kutoka nchini Uganda ni wa pili kwa mabao 19, akifuatwa na mchezaji mwingine wa kigeni Donald Ngoma wa Yanga ambaye amefunga mabao 17.

Mtanzania Elias Maguri anayeichezea Stand United, amefunga mabao 14 huku mchezaji mwingine wa kigeni Kipre Tchetche kutoka Cote Dvoire akimaliza tano bora kwa mabao 12.

Orodha ya wachezaji wa kigeni wanaocheza ligi kuu Tanzania bara msimu 2015/16

niyonzima-3

Yanga FC

.Amis Tambwe-Burundi

.Mbuyu Twite-DRC

.IssofouBourbacar Garba-Niger

.Harun Niyonzima-Rwanda

.Vincent Bossou-Togo

.Thaban Kamusoko-Zimbabwe

.Donald Ngoma-Zimbabwe

Simba FC

Kizza

 

Mara ya mwisho Simba FC kushinda ligi kuu Tanzania bara ilikuwa ni msimu wa mwaka 2011 na 2012.

Katika historia ya klabu hii imeshinda mataji 18.

Wachezaji wa kigeni

Kipa Vincent Angban- Cote Dvoire

Emery Nimubona-Burundi

Hamis Kiiza-Uganda

Juuko Murshid-Uganda

Brian Majwega-Uganda

Justice Majabvi-Zimbabwe

Raphael Kiongera-Kenya.

Azam FC

kipre-tchetche

Inaelekea kumaliza ligi kwa nafasi ya pili kama ilivyokuwa msimu uliopita.

Ilianza kucheza ligi kuu msimu wa mwaka 2008/9 na kushinda taji lake la kwanza na pekee mwaka 2014.

Kocha wake Stewart Hall raia wa Uingereza ambaye kwanza aliwahi kuifunza klabu hiyo kati ya mwaka 2010 hadi 2012 na kurejea tena mwaka 2013 lakini pia mwaka jana, amesema anaondoka katika kalbu hiyo.

Wachezaji wa kulipwa

Pascal Wawa-Cote Dvoire

Allan Wanga-Kenya

Didier Kavumbangu-Burundi

Jean Mugiraneza-Rwanda

Kipre Tchetche-Cote Dvoire

Kipre Bolou-Cote Dvoire

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in