Connect with us

By Fadhili Omari Sizya,

 

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” wameendelea na mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterans kujiandaa na mchezo wa kufuzu Afcon dhidi ya Uganda utakaochezwa Septemba 8,2018 nchini Uganda.

Miongoni mwa wachezaji hao ni maingizo mapya ambapo Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania(Taifa Stars) Emmanuel Amunike aliwaongeza baada ya wachezaji wengine  kushindwa kuwahi kuripoti kambini.

Wachezaji walioitwa kwenye timu ya Taifa walitakiwa kuripoti Jumatatu jioni Agosti 27,2018 isipokuwa wachezaji wa Young Africans waliokabiliwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na wale wanaocheza soka nje ya Tanzania.

Wachezaji walioondolewa kikosini ni Erasto Nyoni,Shomari Kapombe,Jonas Mkude, Ramadhan Kichuya,John Bocco,Hassan Dilunga wote Simba na Feisal Salum wa Young Africans.

Feisal ameondolewa kwa kushindwa kuripoti kambini kwa kuwa hakuongozana na klabu yake ya Young Africans kwenda nchini Rwanda kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho kutokana na kutokuwa na leseni ya kucheza mashindano hayo hivyo alitakiwa kuripoti kambini kama alivyotakiwa.

Wachezaji walioitwa kuziba nafasi hizo ni Salum Kimenya(Tz Prisons)Paul Ngalema,(Lipuli),Frank Domayo(Azam FC),Salum Kihimbwa(Mtibwa),Kelvin Sabato(Mtibwa)David Mwantika(Azam FC) na Ally Abdulkarim(Lipuli)

Wachezaji hao wameungana na wengine walioitwa Taifa Stars kukamilisha kikosi cha wachezaji 25.

Wachezaji wengine walioitwa awali ni

Aishi Manula(Simba)

Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania )

Beno Kakolanya (Young Africans)

Hassan Kessy (Nkana)

Gadiel Michael (Young Africans)

Abdi Banda (Baroka)

Kelvin Yondan (Young Africans)

Aggrey Morris Lipuli(Azam FC)

Andrew Vicent (Young Africans )

Himid Mao (Petrojet)

Mudathir Yahya (Azam FC)

Simon Msuva (Al Jadida)

Rashid Mandawa (BDF)

Farid Mussa (Tenerife)

Feisal Salum (Young Africans)

Mbwana Samatta (Genk)

Thomas Ulimwengu (Al Hilal)

Shabani Chilunda (Tenerife)

Yahya zaydi(Azam FC).

Attachments area

 

More in