Connect with us

 

Wadau wa soka barani Afrika wanahimiza amani nchini Sudan Kusini baada ya vifo vya watu zaidi ya 300 baada ya kutokea kwa makabiliano makali kati ya wanajeshi wanaomuunga mkono rais Salva Kiir na wale wanaomtii Makamu wake wa kwanza Riek Machar.

Kupitia #FootballforpeaceSouthSudan, wadau hao wanataka viongozi wa nchi hiyo kuacha vita na kutambua kuwa mchezo wa soka unaweza kutumiwa kuhamamisha amani nchini humo.

Collins Okinyo mwanahabari wa mchezo wa soka barani Afrika na mwanzilishi wa kundi la Whatsapp la Football Africa Arena akiwa jijini Nairobi nchini Kenya amesema hii ni nafasi ya kuonesha uongozi wa Sudan Kusini kuwa mchezo wa soka unaweza kulete amani.

Leo tunataka kutumia nafasi hii kuanzia kwa viongozi wa Mashirikisho katika mataifa barani Afrika, kutumia mitandao ya Twitter, Facebook na sehemu nyingine kuhimiza amani nchini humo kupitia mchezo wa soka,” alisema Okinyo.

Viongozi wa Sudan Kusini watumie busara kumaliza tofauti zao kwa amani, kwa sababu umwagaji damu hautawafikisha popote #FootballforpeaceSouthSudan,” ameandika rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania Jamal Malinzi.

Rais Salva Kiir na Riek Machar: TAFADHALI FIKIRIA MAISHA ya wananchi wa Sudan Kusini,” aliandika mdau mwingine na mwanahabari wa michezo kutoka Nigeria Osasu Obayiuwana #FootballforpeaceSouthSudan.

Maafisa wawili wa klabu ya Atlabara William Batista na Leko Nelson waliuawa katika mapigano hayo mwishoni mwa juma lililopita.

More in