Leicester City FC ndio mabingwa wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza mwaka 2015/16
Historia ya klabu hii ilianza mwaka 1884 na inatimiza miaka 132.
Inafahamika kwa jina maarufu la The Foxes
Uwanja wake wa nyumbani ni King Power mjini Leicester.
Kocha ni Claudio Ranieri kutoka Italia.
Mmiliki na Mwenyekiti wa klabu hii ni tajiri Vichai Srivaddhanaprabha raia wa Thailand anayemiliki kampuni ya maduka ya bidhaa visivyolipizwa kodi kwa abiria wanaosafiri nje ya nchi wakitokea jijini Bangkong.
Naibu Mwenyekiti wa klabu hii ni Aiyawatt Srivaddhanaprabha mwanaye wa kiume Vichai Srivaddhanaprabha.
Ushindi wa Leicester City umejiri hata kabla ya kukamilika kwa msimu na wadau wa soka wamesema ushindi huu umewashangaza wengi.
Michuano miwili inayosalia ni kati ya Everton tarehe 7 na dhidi ya Chelsea tarehe 15 mwezi huu wa Mei.
Sare ya mabao 2 kwa 2 kati ya Chelsea na Tottenham Hotspurs iliwahakikishia ushindi mashabiki wa Leicester City ubingwa msimu huu.
Klabu hii haikushuka chini ya nafasi ya sita katika jedwali la ligi kuu ya soka msimu mzima na ilichukua usukani mwezi Januari baada ya kuishinda Tottenham bao 1 kwa 0.
Msimu uliopita wa mwaka 2014/5 ilimaliza katika nafasi ya 14.
Mara ya mwisho klabu hii kufanya vizuri ilikuwa ni wakati wa mashindano ya daraja la kwanza walipomaliza nafasi ya pili katika msimu wa mwaka 1928-29.
Leicester City sasa itashiriki katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya msimu ujao na itaanza katika hatua ya makundi.