-
-
by
Victor Abuso
Wagombea saba wanaotafuta urais wa Shirikisho la soka duniani FIFA wameanza kampeni kuomba kura kutoka mabara mbalimbali duniani.
Wanne kati ya wagombea hao wiki hii walizuru makao makuu ya mchezo wa soka barani Afrika CAF jijini Cairo nchini Misri kwenda kujitambulisha.
Bara la Afrika ambalo lina nchi 54 lina kura nyingi ukilinganisha na mabara sita ya FIFA na historia, inaonesha kuwa mshindi wa urais wa FIFA ni lazima aungwe kikamilifu na bara la Afrika.
Wagombea hao waliozuru Cairo ni pamoja na Sheikh Salman Bin Ibrahim Al-Khalifa rais wa Shirikisho la soka barani Asia, Mwanamfalme kutoka Jordan Ali Bin Al Hussein, Gianni Infantino Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEAFA na Tokyo Sexwale mfanyibiashara na mwanaharakati kutoka Afrika Kusini.
Orodha ya wagombea wote:
- Prince Ali bin al-Hussein, miaka 39, rais wa Shirikisho la soka nchini Jordan
- Musa Bility, miaka 48, rais wa Shirikisho la soka nchini Liberia.
- Jerome Champagne, miaka 57, Mwanachama wa zamani wa Kamati kuu ya utendaji ya FIFA
- Gianni Infantino, 45, Katibu Mkuu wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA
- Michel Platini, miaka 60, rais wa Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA na Makamu wa rais wa FIFA
- Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, miaka 49, rais wa Shirikisho la soka barani Asia
- Tokyo Sexwale, miaka 62, mwanasiasa, mwanaharakati na mfanyibiashara kutoka Afrika Kusini.
Uchaguzi huo umeratibiwa kufanyika mwezi Februari mwaka 2016.



Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe

Africa Cup of Nations
Teams get tough opponents in AFCON 2025 Draws

Africa Cup of Nations
Tanzania,Uganda in tricky group with Nigeria and Tunisia

Africa Cup of Nations
Tough Afcon Group B as SouthAfrica paired with Egypt,Angola,Zimbabwe
Must See
-
AFRICA
/ 4 years agoSierra Leone FA President Isha Johansen endorses Patrice Motsepe for CAF President
Sierra Leone FA President who also doubles up as CAF Executive Council member Madam...
-
Football
/ 4 years agoIT JUST CAN NOT BE – AN AFRICA FULL OF MORONS?
By John De Mathews, There is an eerie silence around Africa, and it is...