Wakala wa aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya soka ya Ivory Coast na klabu ya Beijing Enterprises nchini China, Cheick Tiote aliyefariki dunia wiki iliyopita akiwa mazoezini, amewataka wana habari kuacha kujadili na kukisia kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo.
Emanuele Palladino ametoa wito na kusisitiza kuwa huu ni wakati wa kuihurumia na kuomboleza na familia ya Tiote na kuacha kujiuliza maswali yasiyo na majibu.
Kifo cha mchezaji huyo wa zamani wa Newcastle nchini Uingereza, alikocheza kwa muda wa miaka saba, kiliwashtua watu wengi na kuleta huzini kubwa kwa wapenzi wa soka duniani.
Mchezaji huyo aliagwa siku ya Jumanne huku mwili wake ukitarajiwa kurejeshwa nyumbani siku ya Alhamisi kwa taratbu zingine za mazishi.
Cheick Tiote aliichezea nchi yake mara 52 na kuisaidia kunyakua taji la bara Afrika 2015.