Connect with us

Yanga FC kutafuta kurejea kileleni, huku Gor wakichuana na Tusker

Yanga FC kutafuta kurejea kileleni, huku Gor wakichuana na Tusker

 

Michuano ya soka ya ligi kuu nchini Tanzania, Kenya na Uganda inaendelea mwishoni mwa juma hili katika viwanja mbalimbali.

Nchini Tanzania, mchuano mkubwa utakuwa ni kati ya mabingwa watetezi Yanga watakaokuwa wenyeji wa Mtibwa Sugar katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mchuano huu ni muhimu kwa Yanga ambao wanahitaji ushindi ili kurejea kileleni mwa ligi kuu.

Kwa sasa vijana hao wa Jagwani ni wa pili kwa alama 56 baada ya mechi 23 nyuma ya mabingwa wa zamani Simba ambao wanaongoza kwa alama 57 baada ya kucheza mechi 24.

Yanga ikiandikisha ushindi siku ya Jumamosi, itakuwa kileleni kwa ligi alama alama 59 alama 2 zaidi ya Simba ambao walishinda ligi mwaka 2012 na siku ya Jumapili watamenyana na Toto Africans.

Ratiba nyingine Jumamosi:-

  • Coastal Union vs Ruvu Stars
  • Ndanda vs Kagera

Nchini Uganda, mambo yatakuwa yayo hayo katika viwanja mbalimbali jijini Kampala na kwingineko.

Viongozi wa ligi KCCA watakuwa wenyeji wa JMC Hippos huku Express wakivaana na Lweza FC.

KCCA inaongoza ligi hiyo kwa alama 29 baada ya mechi 15 mbele ya Vipers ambayo ina alama 28, huku Police ikiwa ya tatu kwa alama 26.

Ratiba Kamili siku ya Jumamosi:-

  • Express vs Lweza FC
  • Sadolin Paints vs Maroons
  • The Saints vs Police
  • Soana vs URA.

Nchini Kenya katika ligi la Sportspesa, mabingwa watetezi Gor Mahia watakuwa ugenini kuchuana na mabingwa wa zamani na viongozi wa ligi Tusker FC.

Tusker FC kwa sasa inaongoza ligi hiyo kwa alama 17 baada ya mechi 8 na itakuwa katika uwanja wa Nyayo jijini Naiorbi kupambana na mabingwa hao watetezi ambao ni wa 8 katika msururu wa ligi kwa alama 11.

Mjini Awendo Magharibi mwa Kenya, kutakuwa na mpambano wa wanasukari Sony Sugar watakuwa nyumbani kumenyana na Chemelil Sugar.

Muhoroni Youth watawakaribisha Western Stima huku Bandari FC wakiwa wenyeji wa Posta Rangers katika uwanja wa Mbaraki mjini Mombasa.

Ratiba ya Jumapili:-

  • Ulinzi Stars vs Mathare United
  • Thika United vs City Stars
  • Sofapaka FC vs Kakamega Homeboyz
  • Ushuru vs AFC Leopards.

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in