Connect with us

Hili limejiri baada ya timu hii kutoka jijini Dar es salaam, kutoka sare ya kutofungana na Zanaco ya Zambia katika mchuano wa marudiano uliochezwa siku ya Jumamosi jijini Lusaka.

Yanga inayofunzwa na Mzambia George Lwandamina, ilihitaji ushindi wa angalau bao moja na kuepuka sare ili kusonga mbele katika hatua ya makundi.

Juma lililopita, Zanaco wakicheza ugenini  jijini Dar es salaam, ililazimika sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yaliweka pabaya mahesabu ya Yanga na hivyo Zanaco kufuzu kwa bao la ugenini.

Matokeo haya yatawahuzunisha kwa muda mrefu mashabikiwa Yanga  huku kibarua cha kocha wake sasa kikionekana kuwa hatarini.

Mwaka uliopita, Yanga ilifika katika hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho baada ya kuondolewa katika michuano ya klabu bingwa Afrika.

Mbali na matokeo haya mabaya, Yanga imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo, nafasi yao ya kutetea ligi kuu Tanzania bara ikiwa hatarini lakini pia kuendelea kukabiliwa na changamoto za kifedha.

Kumekuwa na madai kuwa, wachezaji wamekuwa hawalipwi marupurupu yao kwa wakati, suala ambalo limesababisha matokeo haya.

Mbali na Yanga, KCCA ya Uganda  pia kutoka Afrika Mashariki imeondolewa katika michuano hii baada ya kufungwa na mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2.

Mchuano wa kwanza uliochezwa nchini Afrika Kusini, Mamelodi ilipata ushindi wa mabao 2-1 lakini mchuano wa marudiano jijini Kampala katika uwanja wa Philip Onyango, timu zote mbili zilitoka sare ya bao 1-1.

KCCA ilihitaji angalao mabao 2-0 ili kusonga mbele katika michuano hii.

 

 

More in