Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga FC wanamenyana na African Sports katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumanne jioni.
Yanga ambao ni wa pili katika msururu wa ligi kwa alama 47, nyuma ya Yanga FC wanahitaji ushindi ili kurejea kileleni mwa ligi hiyo.
Vijana hao wa Jangwani kutoka jijini Dar es salaam hata hivyo, watamkosa nahodha na beki wao wa kati Nadir Haroub kwa jina maarufu Cannavaro ambaye anauguza jeraha, huku wachezaji wengine kama Haruna Niyonzima na Salum Telela akirejea katika mchezo wa leo baada ya kupata nafuu.
Kocha wa African Sports Ramadhan Aluko anasema vijana wake hawajajiandaa vizuri lakini wako tayari kuikabili Yanga na kukubali matokeo yatakavyokuwa.
Simba ambayo inaongoza ligi hiyo kwa alama 48, ilipata ushindi wake muhimu baada ya kuishinda Mbeya City mabao 2 kwa 0 mwishoni mwa juma lililopita.
Ratiba hiyo itaendelea siku ya Jumatano, Tanzania Prisons watamenyana na Kagera Sugar, Coastal Union dhidi ya Mgambo JKT, Mwadui FC itacheza na Majimaji huku JKT Ruvu dhidi ya Toto Africans.
Siku ya Alhamisi, viongozi wa ligi Simba watachuana na Ndanda FC huku Mbeya City wakimaliza kazi na Stand United.