Connect with us

Yanga na Azam FC waendelea kufukuzana ligi kuu Tanzania bara

Yanga na Azam FC waendelea kufukuzana ligi kuu Tanzania bara

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga FC, wanaendelea kuongoza msururu wa ligi kwa alama 15 baada ya kucheza mechi tano msimu huu.

Mabingwa wa zamani Azam FC pia wana alama 15 na wanashikilia nafasi ya pili katika msururu huo wakifuatwa na Simba ambao wana alama 12 sawa na Mtibwa Sugar.

Baada ya michuano sita ya baadhi ya vlabu kutokana na mechi zilizochezwa mwishoni mwa juma, JKT Ruvu wanashikilia nafasi ya mwisho ya 16 kwa alama 1.

African Sports ni ya 14 kwa alama 3 sawa na Coastal Union ambayo ni ya 15.

Mwishoni mwa juma lililopita, Toto Africans walipata ushindi wa bao 1 kwa 0 dhidi ya JKT Ruvu huku Stand United nayo ikiilemea mbeya City pia kwa bao 1 kwa 0.

Tanzania Prisons wakiwa ugenini, waliwafunga Kagera Sugar mabao 3 kwa 0.

Jumamosi iliyopita, Mgambo JKT ilitoka sare ya kutofungana na Coastal Union huku Mwadui FC wakipata ushindi muhimu wa bao 1 kwa 0 dhidi ya wenyeji wao Majimaji.

Michuano ya ligi kuu itaendelea tarehe 17 mwezi Oktoba baada ya kumalizika kwa mchuano wa mzunguko wa kwanza kati ya Tanzania na Malawi nyumbani na ugenini kufuzu katika kombe la dunia nchini Urusi mwaka 2018.

Jumamosi Oktoba 17 2015

Coastal Unio vs Mtibwa Sugar

Stand United vs Tanzania Prisons

Ndanda vs Toto African

Mbeya City vs Simba FC

Majimaji vs African Sports

Yanga vs Azam

Jumapili Oktoba 18 2015

Mgambo JKT vs Kagera Sugar

Mwadui vs JKT Ruvu

Msimamo wa ligi kuu:

#

TIMU

M

AL

1 Young Africans 5 15
2 Azam FC 5 15
3 Simba SC 5 12
4 Mtibwa Sugar 5 12
5 Tanzania Prisons 6 10
6 Toto Africans 6 9
7 Stand United 6 9
8 Mwadui FC 6 8
9 Mgambo JKT 6 8
10 Majimaji 6 7
11 Ndanda FC 5 5
12 Kagera Sugar 6 5
13 Mbeya City 6 4
14 African Sports 5 3
15 Coastal Union 6 3
16 JKT Ruvu 6 1

 

Bedjos Solutions Bondo

Must See

More in