Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga FC walianza vema kampeni ya kutetea ubingwa wake kwa ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchuano wa ufunguzi uliopigwa katika uwanja Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa juma lililopita.
Mabao ya Yanga yalitiwa wavuni na Simon Msuva mfungaji bora wa msimu uliopita huku Donald Ngoma akiipa timu yake bao la pili muda mfupi kabla ya muda wa mapumziko.
Coastal Union ilionekana kuimarika zaidi kipindi cha pili na kujaribu kulishambuliwa lango la Yanga wakati wa mchuano huo ikilinganishwa na msimu uliopita walikofungwa mabao 8 kwa 0 na wanajagwani hao wakati wa mchuano wa ligi kuu.
Yanga wanarejea tena uwanjani siku ya Jumatano kupambana na Tanzania Prisons katika mchuano wake wa pili msimu huu.
Matokeo mengine mwishoni mwa wiki lililopita:
Jumamosi Septemba 12 2015 |
||||
Toto Africans |
1 |
0 |
Mwadui FC |
|
Stand United |
0 |
1 |
Mtibwa Sugar |
|
Azam FC |
2 |
1 |
Tanzania Prisons |
|
Majimaji |
1 |
0 |
JKT Ruvu |
|
African Sports |
0 |
1 |
Simba SC |
|
Ndanda FC |
1 |
1 |
Mgambo JKT |
|
Mbeya City FC |
0 |
1 |
Kagera Sugar |
Ratiba inayofuata:-
Jumatano Septemba 16 2015 |
|||
Young Africans |
vs |
Tanzania Prisons |
|
Mgambo JKT |
vs |
Simba SC |