Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Yanga wamebanwa mbavu baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Singida Uniterd kwenye mchezo wa Ligi Kuu.
Pambano hilo limechezwa kwenye Uwanja wa Namfua Mkoani Singida na kuchezeshwa na mwamuzi Emanuel Mwandembwa wa Arusha.
Timu zote mbili zilionyesha mchezo mzuri ambapo Yanga ilikuwa imara kipindi cha kwanza wakati Singida United walitawala kiupindi cha pili cha mchezo.
Mshambuliaji Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa wa Yanga walishindwa kuipenya ngome ya Singida United huku mshambuliaji raia wa Rwanda Danny Usengimana naye akishindw akufua dafu mbele ya walinzi wa Yanga walioongozwa na Andrew Vicent na Kelvin Yondan.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha alama 17.
Nahodha wa Singida United Mudathir Yahya amesema timu yake ilicheza vizuri lakini ilishindwa kupata ushindi kutokana na ugumu wa mchezo.
“Tulicheza vizuri lakini hatukufunga, dhamira yetu ilikuwa kushinda lakini tunashukuru kwa matokeo haya,’amesema
Kiungo wa Yanga, Pato Ngonyani amesema Ligi ya msimu huu ni ngumu kwa kuwa kila timu inayoshuka dimbani inahitaji alama tatu.