Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Pamoja na kuwa na uzoefu mkubwa katika michuano ya kimataifa ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup Yanga SC imeonekana kuchukua tahadhari zaidi kuelekea mchezo wao wa play off dhidi ya Pyramids FC wa kuwania kucheza hatua ya Makundi ya CAF Confederation Cup kwa kuhama uwanja.
Yanga baada ya kupangwa na Pyramids FC ya Misri ambao wanatajwa kuwa na kikosi ghali zaidi huku wakidaiwa kuwahi kufanya uthubutu wa kumsajili mchezaji mmoja kutokea Brazil Marcos Keno kwa dau la dola za kimarekani milioni 10.
Inadaiwa wameamua kuihamisha mechi yao ya Oktoba 27 2019 katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza na sio uwanja wa Taifa Dar es Salaam, kwa mujibu wa Yanga wamedai wamefanya hivyo ili kuwapa burudani mashabiki wake wa mikoani ila tetesi cha chini ya kapeti zinadai kuwa Yanga wamefanya maamuzi hayo kwa sababu mbili kwa kupeleka mchezo katika uwanja ambao Pyramids FC watasumbuka kuutumia lakini pili kukimbia presha za mashabiki wa wapinzani wao wa jadi Simba ambapo siku hiyo ya October 27 wataishangilia Pyramids.