Yanga imeanza vibaya mchezo wa hatua ya kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Township Rollers katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanawapa wakati mgumu Yanga kabla ya mchezo wa marudiano baina ya timu hizo utakaochezwa Mjini Gaberone nchini Botswana.
Mabao ya Rollers yalifungwa na Lempose Tshireletso dakika ya 11 kwa shuti kali lililomshinda kipa wa Yanga, Ramadhan kabwili huku bao la pili likifungwa na Motsholetsi Sokwe kipindi cha pili baada ya wachezaji wa timu hiyo kugongeana pasi zaidi ya 10 kabla ya mpira kumfikia mfungaji.
Bao la kufutia machozi la Yanga lilifungwa na mchezaji kutoka Zambia, Obrey Chirwa dakika ya 30 yamchezo akimalizia pasi kiungo Papy Tshishimbi.
Matokeo ya michezo mingine ya Ligi ya mabingwa Afrika
Al Ahly ya Misri iliishinda FC Mounana ya Gabon kwa mabao 4-0
FC Horoya ya Guinea iliichapa Generation ya Senegal mabao 2-1
Etoile Sahel iliishinda Plateau mabao 4-2.
Ratiba ya michezo ya leo ni kama ifuatavyo
Gor Mahia ya Kenya inaipokea Esperance ya Tunisia
Saint George ya Ethiopia inachuana na KCCA ya Uganda
Zanaco ya Zambia inacheza na Mbabane Swallows ya Swaziland
Rayon Sports inachuana na Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini
Difaa Jadida ya Morocco inachuana na AS Vita Club ya DRC
TP Mazembe inacheza na UD Songo ya Msumbiji
Zesco ya Zambia inacheza na Asec Mimosas ya Ivory Coast