Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya taji la Shirikisho Afrika, Yanga wamepangwa kuchuana na timu za Rayon sports ya Rwanda, Gor Mahia ya Kenya na USM Alger ya Algeria katika Kundi D la michuano hiyo.
Droo ya michuano hiyo imefanyika leo katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika CAF mjini Cairo nchini Misri.
Kundi A lina timu za ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Raja Casablanca ya Morocco, AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Adouana Stars ya Ghana.
Kundi B lina timu za Renaissance Sportive De Berkane ya Morocco, El Masry ya Misri, El Hilal ya Sudan na Uniao Desportiva da Sango ya Msumbiji.
Kundi C la michuano hiyo ya pili kwa ngazi ya klabu barani Afrika lina timu za Enyimba ya Nigeria, Williamsville ya Ivory Coast, Club Athletique Rennaissance Algions ya Congo.
Mechi za hatua ya makundi zinatazamiwa kuanza mwezi wa Juni.
Timu mbili za juu kwa kila kundi zitafuzu kucheza hatua ya nusu fainali.