Na Mwandishi wetu akiwa Dar Es Salaam,
Kamati ya utendaji ya timu ya Yanga SC inayoongozwa na mwenyekiti wa klabu hiyo DR Mshindo Msolla mapema wikii ilimfukuza kazi rasmi aliyekuwa kocha wao mkuu Mwinyi Zahera raia wa Congo.
Yanga walimfuta kazi Zahera siku moja baada ya kutolewa Kombe la shirikisho Afrika na Pyramids FC ya nchini Misri kwa kufungwa jumla ya magoli (aggregate) 5-1, sasa baada ya kurejea Tanzania tu Yanga wakamfuta kazi kocha wao na kuvunja benchi la ufundi.
Wengi wanashangaa maamuzi ya Yanga kufikia hatua hiyo, kwani hadi sasa Zahera (2019/2020) katika michezo yote 10 aliyoiongoza Yanga ameshinda mitatu, sare 3 na kupoteza mechi 4.
Kwa upande wa jumla Zahera ambaye ana mwaka mmoja na nusu toka alipowasili Yanga Aprili 24 2018, ameifundisha Yanga katika michezo 63, akishinda mechi 32, amefungwa mechi 21 na sare mechi 10.