Klabu ya soka ya Zamalek FC kutoka nchini Misri, imetangaza kujiondoa katika ligi kuu ya soka nchini humo kwa madai ya kuonewa na refarii.
Uongozi wa klabu hii umekuja baada ya kufungwa na klabu ya Tala’ea El-Gaish mabao 3 kwa 2 katika mchuano wa ligi kuu mwishoni mwa juma lililopita.
Mabingwa hao watetezi wa ligi kuu nchini humo, wamesema hatua ya refarii wa kati kumpa kadi nyekundu beki wao Ali Gabr na kuipa Tala’ea mkwaju wa penalti ilikuwa ni makosa.
Kabla ya mchuano huo, uongozi wa klabu hiyo inasema ilikuwa imemlalamikia mwamuzi wa kati aliyechezesha mchuano huo Mahmoud al-Banna.
“Inaonekana, kulikuwa na lengo la kumkabidhi na kumteau Banna mchuano huu ili kuionea Zamalek,” taarifa ya Zamalek imeeleza.
Zamalek imejiondoa katika ligi hiyo huku ratiba ya ligi kuu nchini humo ikitarajiwa kuwa dhidi ya Ghazl El Mahalla siku ya Jumatano.