Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati limetoa orodha ya kikosi bora cha mashindano hayo huku Timu ya Taifa ya Zanzibar ‘Zanzibar Heroes’ ikitoa wachezaji wawili.
Wachezaji hao ni beki wa Kushoto Mwinyi Haji Mngwali na Kiungo Abdul Aziz Makame. Wachezaji wengine waliopo kweny orodha hiyo ni Kipa Patrick Matasi ambaye aliokoa penati tatu katika mchezo wa fainali baina ya Kenya na Zanzibar.
Kilimanjaro Stars ambayo iliishia hatua ya makundi imetoa mchezaji mmoja Himid Mao ambaye ameingia kwenye kikosi cha akiba.
Wachezaji wengine waliopo kwenye kikoi bora ni Fitina Omborenga (Rwanda), Jockins Atudo (Kenya),Bernard Muwanga (Uganda), Alharaish Zakaria (Libya),Patillah Omoto (Kenya), Derrick Nsibambi (Uganda), Shassir Nahimana (Burundi), Abubakher Sanni (Ethiopia).
Kikosi cha akiba kinaundwa na Abdulrahman Mohamed (, Zanzibar), Yaleh Tilahun (Ethiopia), Himid Mao (Tanzania Mainland), Milton Kalisa (Uganda), Hakizimana Muhadjiri (Rwanda), Issa Juma, Feisal Abdalla and Mudathir Yahya (Zanzibar), Wol Atak (South Sudan), Dennis Sikhai, Masud Juma, Vincent Oburu (Kenya), Taktak Muftah (Libya).
Tuzo ya Kocha bora wa michuano hiyo imechukuliwa na Hemed Morocco wa Zanzibar heroes huku msaidizi wake akiwa Paul Put wa Kenya.