Connect with us

 

Michuano ya soka ya ligi kuu katika nchi za Afrika Mashariki ziliendelea kutimua vumbi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Nchini Kenya katika ligi ya Sportspesa, Klabu ya Sofapaka ambayo ipo katika hatari ya kushushwa daraja ililazimisha sare ya kutofungana na mabingwa watetezi Gor Mahia.

Matokeo haya yanaifanya Sofapaka kusalia katika nafasi ya mwisho ya 16 kwa alama 7.

Tangu kuanza kwa msimu huu, Sofapaka imeshinda mechi 2 kati ya 15 ilizocheza hadi sasa na kufungwa mechi 12 huku mchuano mmoja ikitoka sare.

Gor Mahia inashikilia nafasi ya nne kwa alama 26, nyuma ya Ulinzi Stars na Mathare United ambazo zote zina alama 27.

Mabingwa wa mwaka 2012 Tusker FC, wanaongoza jedwali la ligi kwa alama 29.

Katika ligi ya Tanzania bara, nchini Tanzania, Stand United kutoka Shinyanga imepanda hadi katika nafasi ya pili kwa alama 12 baada ya kuwaangusha mabingwa watetezi Yanga FC kutoka Dar es salaam bao 1-0.

Hii ndio ilikuwa mara ya kwanza Stand United kuifunga Yanga katika historia yake.

Yanga ni ya tatu kwa alama 10 sawa na Azam FC, huku mabingwa wa zamani Smba FC wakiongoza jedwali kwa alama 16 baada ya mechi sita msimu huu.

Tarehe 1 mwezi Oktoba, miamba wa soka nchini humo Simba na Yanga watamenyana katika mchuano muhimu wa ligi kuu utakaopigwa jijini Dar es salaam.

Nchini Uganda, mabingwa watetezi KCCA waliendelea kufanya vizuri baada ya kuishinda BUL C mabao 3-1.

Matokeo mengine:-

Lweza 2-1 JMC Hippos

Onduparaka FC 2-1 Police 1

Proline 1- 1 URA

Vipers 0-1 Express

Soana 0-0 Bright Stars

Saints FC 1-0 Jinja

More in East Africa